Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Wilaya ya Kyerwa imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Kyerwa leo Januari 19, 2024.
Katika ziara hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Mhe. Bahati Henerico imekagua ujenzi wa Zahanati ya Katera, ujenzi wa Uzio wa Mnada wa ng’ombe katika Kijiji cha Katera Kata ya Isingiro na mradi wa ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa lililopo Rwenkorongo Kata ya Kyerwa.
Vile vile kamati imetembelea na kukagua Nyanda za Malisho ya Siina, na Kizuizi cha Kaitambuzi Vilivyoko katika Kata ya Isingiro.
Kamati imepongeza utekelezaji wa miradi hiyo na kushauri ikamilike kwa wakati ili iweze kuleta tija.
Aidha katika Kizuizi cha Kaitambuzi kamati imeishauri Halmashauri kuwaelekeza wakaguzi wa vizuizi wote kuongeza juhudi katika ukaguzi na usimamizi wa vizuizi vyao.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved