IDARA YA MIFUGO NA UVUVI
FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI WILAYA YA KYERWA
UTANGULIZI
Sekta ya Mifugo na Uvuvi imekuwa miongoni mwa sekta muhimu sana hapa nchini katika kuinua kipato cha mwananchi. Katika Sekta hii wananchi wamejikita katika ufugaji wa ng’ombe, mbuzi, nguruwe, kuku, bata, sungura n.k kwa ajili ya matumizi ya chakula na biashara ili kukidhi mahitaji ya kaya zao. Wilaya ya Kyerwa Wananchi wamejikita zaidi katika ufugaji wa ng’ombe wa asili, mbuzi wa asili na kuku wa asili. Pamoja na wafugaji mmojammoja wananchi pia wanashirikiana kwa kuunda vikundi vidogovidogo vinavyowasaidia na kuwapa mwanya katika kusaidiana katika matatizo mbalimbali ya kijamii.
Sekta ya Mifugo na Uvuvi Wliayani Kyerwa ina fulsa mbalimbali za Uwekezaji ambazo zinaweza kuongeza tija zaidi kwa Wananchi katika kipato cha kila siku na kwa maendeleo ya Wananchi, Wlaya na Taifa kwa ujumla. Zifuatazo ni baadhi ya fursa za Uwekezaji zilizopo katika Sekta hii katika Wilaya ya Kyerwa:-
MUHIMU:-WILAYA YA KYERWA INA HALI NZURI YA HEWA, AMANI, UTAWALA MZURI, HALI NZURI YA HEWA NA UWEPO WA FURSA MBALIMBALI ZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI, HIVYO INAWAKARIBISHA WAWEKEZAJI WA NDANI NA NJE YA WILAYA KUWEKEZA KATIKA MAENEO HAYO.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved