Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, SACF. James John, Januari 19, 2026 ametembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Idara ya Afya inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Miongoni mwa miradi iliyokaguliwa ikiwemo Ujenzi wa Wodi ya Wazazi (Jengo la mama na mtoto) katika Kituo cha Afya Rutunguru, Maandalizi ya ujenzi wa nyumba ya watumishi wa Afya Nyakashenyi, ujenzi wa Zahanati mpya Businde na ujenzi wa Wodi ya wazazi (Jengo la mama na mtoto) pamoja na ujenzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo Cha Afya Mabira.
Miradi mingine ni ukamilishaji wa chumba cha kliniki ya watoto na vyumba vya madaktari katika Zahanati ya Rwanyango, ujenzi wa chumba cha kujifungulia katika Zahanati ya Kakanja na ujenzi wa Zahanati ya Kaina.
SACF. James alitoa maelekezo mbalimbali kwa kila mradi kulingana na hali yake ikiwemo kuongeza kasi ya ujenzi wa miradi hiyo ili ianze kutoa huduma kwa jamii.Katika ziara hiyo, SACF. James aliambatana na wataalam wa Halmashauri akiwemo; Mganga Mkuu wa Wilaya, Mhandisi wa Wilaya pamoja na Afisa Manunuzi.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Copyright ©2025, ICT Department Kyerwa District Council . All rights reserved.