Halmashauri hufanya manunuzi ya Serikali kwa kufuata taratibu za manunuzi kama zilivyo ainishwa katika sheria ya manunuzi ya mwaka 2011 na kanuni ya manunuzi ya mwaka 2013.
Kwa utaratibu huo,baada ya kuandaa bajeti ya Halmashauri ,kila idara huandaa mpango wa manunuzi wa idara yake kwa kila mwaka wa fedha,lengo la mpango wa manunuzi wa kila idara ni kuhakikisha kuwa manunuzi ya Serikali yanafanyika kwa kuzingatia kanuni na taratibu za Serikali na pia kuonyesha thamani ya pesa kwa kila bidhaa au huduma iliyotolewa na kupunguza gharama za manunuzi.
Kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ilikisia kutumia kiasi cha Tzs 7,547,351,843 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na huduma,kazi za kihandisi,pamoja na huduma za ushauri wa kitaalam.
Katika mwaka huu wa fedha 2016/2017 Halmashauri inatekeleza miradi tisa ya barabara,ujenzi wa jengo la ofisi ya utawala makao makuu ya Halmashauri,na kazi ya ushauri wa kitaalam katika mradi wa maji katika vijiji 57 Wilayani kyerwa.Pia upande wa afya halmashauri inatekeleza ujenzi wa jengo la wajawazito katika kituo cha afya Nkwenda.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved