Utoaji wa huduma ya elimu katika Wilaya ya Kyerwa uazingatia sheria,sera,na miongozo mbalimbali kama vile sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 1996,Sheria ya Elimu Na.25 ya mwaka 1978 na marekebisho ya sheria Na.10 ya mwaka 1995.Wilaya inatambua kuwa watu wenye elimu ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu na hakiya kupata elimu inatambulika kisheria katika katiba yetu.
Elimu ya msingi bila malipo
Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa inasimamia na kutekeleza huduma ya utoaji wa elimu ya msingi bila malipo.Katika utoaji wa huduma hii,wanafunzi hupata elimu bila ya kuchangia fedha.Fedha za uendeshaji wa shule hutolewa na serikali.Kwa mwaka wa fedha 2015/2016 jumla ya tsh 241,101,000 imepokelewa kwenye shule za msingi,na kiasi cha tsh 413,233,553 kimepokelewa kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Aidha wananchi wanashirikiana na serikali yao kwa kuchangia nguvu za jamii katika miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu ya shule.
P4R
Huu ni mpango unaojulikana kamampango wa elimu kwa ajili ya matokeo(MEam).Mpango huu katika Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa kwa mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/2017 umesaidia sana katika maeneo yafuatayo:-
Aidha,jumla ya Tsh 78,000,000 zilipokelewa kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ,na jumla ya Tsh 271,006,960 zilipokelewa kwa mwaka wa fedha 2016/2017.Fedha hizi zimesaidia kufanikisha maeneo yaliyotajwa hapo juu.
Usajili wa darasa la kwanza
Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa imefanikiwa kuongeza kiwango cha usajili wa wanafunzi wa darasa la kwanza ikilinganishwa na miaka ya nyuma.Mwaka 2016 ilikadiriwa kusajili wavulana 4525,na wasichana 4319
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved