Idara ya Ujenzi inayo jukumu kubwa la kutoa ushauri na kusimamia shughuli zote za idara katika sekta za barabara,majengo kwa taasisi na idara za Serikali,Sekta binafsi,pamoja na wananchi kwa ujumla.Lengo kubwa ni kuhakikisha kuwa shughuli zote katika vitengo mbalimbali vya idara vinasimamiwa kiufanisi.
Vilevile idara ya Ujenzi inahusika na kutoa ushauri kwa Halmashauri kuhusiana na masuala ya umeme,mitambo,na Zimamoto.Aidha,Kimuundo idara ya Ujenzi inavyo Vitengo vinne (4) ambavyo ni:Barabara,Majengo,Mitambo na Umeme,Zimamoto.
Mtandao wa Barabara
Wilaya inazo jumla ya km 738.90 za barabara.Kati ya hizo Km 126.0 ni za Wilaya, na Km 606.9 ni za Vijiji, na Km 6.0 ni barabara nyingine.Barabara nyingi zinapitika vizuri kwa kipindi chote cha mwaka isipokuwa kwa baadhi ya maeneo machache ambayo yanapitika kwa shida wakati wa vipindi vya mvua hususani barabara zenye viwango vya udongo.
Ili kuzihudumia barabara hizi, Halmashauri imekuwa ikitenga kiasi cha pesa katika mpango wake wa bajeti kila mwaka kwa ajili ya ukarabati wa maeneo korofi,matengenezo maalumu ya barabara, na kufufua barabara mpya.
Majengo
Idara huusika na usimamizi wa majengo ya Serikali ili yaweze kujengwa kwa ubora unaotakiwa.Kitengo kwa kushirikiana na idara mama kimekuwa kikitoa ushauri na kufanya usimamizi wa ujenzi wa majengo yanayoendelea kujengwa.
Mitambo na Umeme
Kitengo hiki kina jukumu la kusimamia mashine na mitambo inayomilikiwa na Halmashauri.Magari na vyombo vingine vya moto vimekuwa vikisimamiwa na kitengo hiki kwa matengenezo na uratibu wake kwa ushirikiano na kitengo cha usafirishaji.
Kwa kuwa Halmashauri haina karakana ya magari, kitengo kimekuwa kikifanya ukaguzi na uhakiki wa matengenezo ya mitambo /magari na kuishauri Halmashauri.
Zimamoto
Utokeaji wa majanga ya moto na athari zake yamekuwa yakidhibitiwa na idara hii kwa kushirikiana na taasisi nyingine za usalama.Pamoja na umuhimu wake katika jamii kitengo hiki bado kinakabiliwa na changamoto nyingi hasa za vitendea kazi,na wataalamu.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved