Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Mhe. Bahati Henerico amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Tawi la Mkoa wa Kagera kwa kipindi Cha miaka mitano ijayo.
Mwenyekiti huyo wa ALAT Mkoa wa Kagera amechaguliwa Leo katika uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Bukoba ambapo amepata kura 24 dhidi ya kura 8 alizopata mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Muleba Mhe. Justus Magongo.
Akiongea mara baada ya kuchaguliwa kwa wadhifa huo, Henerico amewaomba wajumbe wa kikao hicho, Wenyeviti na Wakurugenzi Watendaji ushirikiano wa dhati ili kuendesha gurudumu hilo zito lililombele yake.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Copyright ©2025, ICT Department Kyerwa District Council . All rights reserved.