Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango (FUM) ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Januari 22, 2026 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi sita (6) ya maendeleo yenye thamani ya Sh. 1,140,181,159 inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Akiongoza ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Mhe. Bahati Henerico amepongeza utekelezaji wa miradi iliyotembelewa huku akiwashukuru wataalam wa Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo kwa ujumla.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni Ukamilishaji wa Maabara ya Fizikia na Baiolojia katika Shule ya Sekondari Rwabwere, Ujenzi wa Vyumba vinne vya madarasa na matundu 14 ya Vyoo katika Shule ya Msingi Nyarutuntu-Kata ya Nkwenda, Ujenzi wa Jengo la Wodi ya Wazazi katika Zahanati ya Rukuraijo.


Miradi mingine ni Shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Mapinduzi (Mapinduzi English Medium) na Ujenzi wa Shule ya Msingi Mpya ya Kyerwa Modern Kata ya Kyerwa pamoja na Kikundi cha Muungano Vijana Kyerwa kinachojishughulisha ya Ufyatuaji wa tofali na uuzaji wa madini ujenzi kinachonufaika na mkopo wa 10% wa Halmashauri.
Baada ya kutembelea na kukagua miradi hiyo, Kamati imeelekeza kumalizia maabara mbili za shule ya Sec. Rwabwere huku ikipongeza usimamizi mzuri wa Mradi wa Shule ya Msingi Nyarutuntu na kupendekeza shule nyingine kwenda kujifinza namna ya kusimamia miradi katika shule hiyo huku ikitaka miradi yote ikamishwe kwa wakati ili ianze kutoa hudumu kwa wananchi.
Vile vile kamati imetoa maelekezo kwa majukwaa ya Wazazi katika shule zote za Wilaya ya Kyerwa kuimarishwa, ili yaweze kutekeleza majukumu yao ikiwemo kisimamia uripotiji wa wanafunzi na miradi, kusimamia michango inayochangwa na wazazi kwa ajili ya maendeleo ya shule isiweze kupotea kwa lengo la kuepusha migongano kati ya wazazi na watumishi.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Copyright ©2025, ICT Department Kyerwa District Council . All rights reserved.