Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti (Mwenye gwanda la JWTZ)atembelea hospitali ya Wilaya ya Kyerwa tarehe 13/06/2019. Mkuu huyo wa Mkoa alifanya ziara Wilayani Kyerwa kukagua maendeleo mbalimbali ikiwa ni pamoja na maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo ya Wilaya. Katika ukaguzi wa ujenzi huo alionekana kuridhishwa na kasi ya ujenzi unaoendelea na kuagiza Wilaya kuhakikisha inamkabidhi hospitali hiyo ifikapo tarehe 25/06/2019 tayari kwa kumkabidhi Mhe. Waziri Ofisi ya Rais- TAMISEMI. Wilaya ya Kyerwa ni moja ya Wilaya kati ya 67 zilizopatiwa fedha sh. Bilioni moja na nusu kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya. Akiendelea na ziara hiyo Mkuu wa Mkoa aliweza kutembelea soko la Kata ya Isingiro kwa lengo la kukagua ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali na matumizi ya vitambulisho hivyo. Aidha aliweza kutembelea maeneo ya mialo ambayo inatumika kutorosha kahawa na mazao mengine kwa njia ya magendo. Katika kutembelea maeneo hayo aliweza kufika eneo la mwalo wa Kashenyi Murongo na kutoa maelekezo kwa viongozi wa Wilaya kuhakikisha wanasaidiana kukomesha biashara hiyo haramu. Pamoja na kutembelea maeneo ya mialo aliweza pia kuongea na wananchi kupitia mkutano wa hadhara katika eneo la Kajumilo kata ya Businde. Katika mkutano huo aliweza kuwaeleza wananchi juu ya msimamo wa serikali kuhusu biashara hiyo haramu na kutoa maelekezo kwa viongozi wa ngazi zote kuhakikisha biashara hiyo inakoma. (Na Golden Nzalalila, Afisa Habari Kyerwa)
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved