Afisa uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, ndugu Yasin Darabe amekamata mitumbwi 17 na nyavu 750 zenye ukubwa wa macho chini ya inchi 3 katika ziwa Ruko kata ya Kitwechenkura. Hayo yamebainika katika doria iliyofanyika kati ya tarehe 1-2 Machi, 2018 baada ya Wilaya kuweka zuio la uvuvi kwa kipindi cha miezi sita toka 3 Januari,2018 hadi 30 Juni,2018.
Aidha, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ruko ndugu Aidan Ismail amebainisha kuwa baadhi ya wavuvi wasio waaminifu wamekuwa wakificha mitumbwi yao wakati wa mchana na kuitumia usiku kinyume na agizo/katazo la Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya,Kanali Mstaafu Shaban I.Lissu. Naye ndugu Augustin John ambaye ni Mwenyekiti wa kikundi cha wavuvi katika mwalo wa Ruko,amesema atahakikisha zana zote haramu zilizopo eneo lake zinakamatwa na kuteketezwa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved