Wilaya ya Kyerwa yaibuka kinara wa ufugaji wa ng'ombe wa maziwa Mkoani Kagera.Ushindi huo umepatikana katika siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya unywaji maziwa kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya nanenane Kyakailabwa,mkoani Kagera kuanzia tarehe 28/5/2017 hadi tarehe 1/06/2017.
Mfugaji ndg Timotheo Kalekayo wa Kijiji cha Nyakatete,kata ya Mabira Wilayani Kyerwa aliibuka mshindi wa kwanza baada ya kuwabwaga wafugaji wenzake kutoka Wilaya nane za mkoa wa Kagera.Mshindi huyu aliyeiletea sifa Wilaya ya Kyerwa alikuwa na ng'ombe aina ya Friesian aliye mtoa katika zizi lake mwenye uzito wa kilogramu 467,uwezo wa kutoa maziwa lita 20 kwa siku,huku akiwa kazaa ndama wawili (2) mapacha .
Pia ushindi wake ndg Timotheo Kalekayo ulichagizwa na ujenzi wa banda bora la kufugia ng'ombe wa maziwa lililokuwa limetengenezwa kiustadi kitendo kilichowavutia wananchi wengi waliotembelea maonyesho hayo kulitazama na kujifunza mambo mbali mbali.
Kwa ushindi huo mgeni rasmi mheshimiwa Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Charles Tizeba (Mb)alimkabidhi mshindi huyu tuzo ya medali ya dhahabu,kombe,cheti cha ushindi,na dumu la chuma(cane) lenye uwezo wa kuhifadhi lita 50 za maziwa. Washindi wengine wa pili na tatu walitoka Wilaya za Missenyi,na Ngara.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved