Mheshimiwa Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu-Jenista Mhagama(Mb) amefanya ziara ya siku moja Wilayani Kyerwa leo tarehe 11 Julai,2017 kwa ajili ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa kupitia fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kurekebisha miundombinu ya zahati ya Rwele iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi.
Serikali imetoa kiasi cha shilingi 125,450,330.00 kwa ajili ya kujenga zahanati mpya ya Rwele ambayo inahudumia takribani wananchi 25,000 katika vijiji sita vya kata ya Kikukuru na maeneo jirani.
Mradi umekamilika katika hatua ya msingi na unaendelea kupandisha kuta.Zahanati hii pindi itakapokamilika itakuwa na OPD,chumba cha mapokezi ya wagonjwa,chumba kimoja cha daktari,chumba kimoja cha kujifungua(Labour),chumba cha akina mama wajawazito kupumzika baada ya kujifungua(Postinal room),na vyumba 02 vya dawa.Pia kutakuwa na chumba cha kupimia wajawazito,chumba cha chanjo,chumba cha vipimo vya maabara,chumba cha sindano,na chumba cha kuhifadhia vifaa.
Huduma zitakazotolewa na zahanati hii ni pamoja na huduma za mama na mtoto,huduma za chachanjo,huduma za maabara,huduma za ushauri nasaa,na huduma za wagonjwa wa nje.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved