MKUU wa wilaya ya kyerwa Mhe. Zaituni Msofe leo tarehe 18 Julai 2023 ametoa wito kwa wazazi na jamii kwa ujumla kutimiza wajibu wa kuwalisha watoto ili kuboresha afya zao.
Amesema hayo katika kikao cha taarifa ya utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa kipindi cha robo ya mwaka kuanzia Aprili hadi Juni Mwaka huu kilichofanyika katika ukumbi wa Rweru Plazza Wilayani Kyerwa.
“Mzazi asikwepe majukumu, tuhakikishe tunawapa chakula watoto wetu. Na kwa wazazi wanaodhani watoto wa darasa la awali na la kwanza hawatakiwi kula shuleni wasiachwe, wapewe elimu ili watoa chakula kwa watoto wao pindi wawapo shuleni.” Alisema Mhe. Msofe.
Ametoa wito kwa wajumbe wa kikao hicho ambao ni watendaji wa kata, watendaji wa Vijiji na waratibu wa elimu na wadau wengine kuhakikisha kikao cha robo ya mwaka kijacho, kila kata iwe imefikia asilimia 85 au zaidi za watoto wanaopata lishe.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved