Ndugu Shadrack Mhagama ,amewasihi watumishi wapya walioajiliwa katika Halmashauri ya Kyerwa,wawatumikie wananchi kwa kujituma na kufuata maadili ya uongozi pindi watakapowasili katika vituo vyao. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mhagama wakati wa mafunzo ya kuwapokea watumishi 61 yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Kyerwa tarehe 26 Mayi, 2018.
Aidha,mafunzo haya yaliyojumuisha watumishi ajira mpya kuanzia ajira za Disemba,2017 hadi Mayi,2018 kwa kada za watendaji wa Vijiji 27,Walimu wa shule za Msingi 24, na watumishi wa Afya 10.
Katika mafunzo hayo mada mbalimbali zilitolewa kuhusu masuala ya utumishi wa umma na kanuni zake,maadili ya utumishi wa umma,masuala ya kijamii,sheria na taratibu za fedha za umma,sheria za manunuzi ya umma,masuala ya ardhi na kanuni zake,na taratibu za ukaguzi wa mali za umma.
Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa iminaupungufu mkubwa wa wataalam katika sekta mbalimbali,kwani kwa sasa ina jumla ya watumishi 1897 tu kati ya mahitaji ya watumishi 3149,hivyo ujio wa watumishi hawa utaongeza ufanisi wa Halmashauri kuwahudumia wananchi
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved