Baadhi ya Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa wamepatiwa mafunzo ya kutumia mfumo wa kielektroniki wa upimaji wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma yaani Public Employee Performance Management Information System (PEPMIS) ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji kwa watumishi wa umma.
Mkurugenzi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Jeanfrida Mushumbuzi akiongoza mafunzo hayo, amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kushughulikia changamoto zinazojitokeza na kufuatilia mwenendo wa utumiaji wa mfumo huo kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa.
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, SACF. James John amewataka washiriki wote wa mafunzo hayo kufuatilia kwa uadilifu na kujifunza kwa makini pamoja na kuyafanyia kazi mafunzo hayo ili lengo la Serikali liweze kutimia.
Mafunzo hayo yanayolenga kuwajengea uwezo watumishi wa umma katika kutumia mfumo huo yametolewa kwa awamu ya pili katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ambapo mafunzo ya awali yalitolewa mwezi Desemba 2023.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved