Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa leo tarehe 30 Septemba 2023 wameshiriki katika bonanza la michezo lilofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kyerwa.
Akifungua bonanza hilo Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe amewapongeza viongozi na watumishi wote wa Halmashauri kwa kuandaa bonanza hilo huku akiwataka kuwa na utaratibu wa kushiriki katika michezo na kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuimarisha afya zao.
Vile vile ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kwa utendaji kazi mzuri na kutoa huduma nzuri kwa jamii na kuwataka kuendelea kujituma na kufanya vizuri zaidi.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa SACF. James John amesema zoezi hilo litakuwa endelevu na litakuwa linafanyika kila mwezi na atapanga utaratibu mzuri ili kila Tarafa za Wilaya ya Kyerwa kuandaa na kushiriki katika mabonanza mbalimbali ya michezo.
Katika bonanza la leo kulikuwa na michezo mbalimbali iliyochezwa na kuwa na matokeo kama ifatavyo; Mpira wa Miguu Team A 1-2 Team B, Partner Football Team A I-0 Team B, kuangamiza Viini Malazi Team A Point 9-12 Team B, na Mbio za Vijiti ukikimbia huku ukiandika neno Umoja ni Nguvu Team B ilishinda, Upwa na Ziwa Team B ilishinda, na Volleyball Team A Set 3-2 Team B na kufanya matokeo ya Jumla kuwa Team B ilifanikiwa kushinda michezo 4 na Team A kushinda Michezo 2.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved