Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Dkt. Lewanga Msafiri leo Oktoba 13, 2025 amefungua mafunzo ya kupambana na ugonjwa wa utapiamlo kwa watoto katika Wilaya ya Kyerwa.
Akifungua mafunzo hayo katika ukumbi wa Halmashauri, amewataka washiriki wote kushiriki kikamilifu ili waweze kujengewa uwezo wa kutambua dalili za utapiamlo na kutibu changamoto za ugonjwa huo kwa watoto katika jamii.
Mafunzo hayo yatafanyika kwa muda wa siku tano yakihusisha watumishi wa afya kutoka katika Vituo vya Afya na Hospitali ya Wilaya ya Kyerwa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved