Wataalam kutoka ABEA walikutana na wafugaji wa ng'ombe wa maziwa na ng'ombe wa asili mnamo tarehe 23 Novemba,2017 kutoka kata za Nkwenda,Kikukuru,,Kimuli,Iteera,Rwabwere,Rukulaijo,na Kitwechenkula.Jumla ya wafugaji 58 walihudhuria.
ABEA ni kifupi cha neno "Animal Breeding East Africa" ,hii ni kampuni ya kimataifa iliyosajiliwa nchini,chini ya sheria ya makampuni (sheria namba 12 ya mwaka 2002).Aidha meneja wa ABEA kanda ya ziwa ndugu Yvonne Robben aliongoza ujumbe wa
wataalam wanne(4).Kutoka ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri wataalam wawili (2),ndugu Prosper Rutakiniwa(Afisa mifugo Wilaya) na ndugu Rhoda Magadula(Mratibu wa tasnia ya maziwa Wilaya) walihudhuria mkutano huo ambapo walishirikiana na viongozi wa mtandao wa umoja wa wafugaji wa ng'ombe wa Maziwa Nkwenda(UNKWERWAKI) kuhamasisha wafugaji kuhudhuria mkutano huo.
Wataalam kutoka "ABEA" walitoa mada juu ya faida za kutumia njia ya uhimilishaji ng'ombe ili kupata ng'ombe bora wa maziwa na kuongeza tija.Aidha,mpango wa kuhimilisha ng'ombe uliwasilishwa kwa wafugaji na baada ya majadiliano kuhusu mpango huo,wafugaji waliupokea na jumla ya ng'ombe 26 wa maziwa walibainishwa ili kuanza shughuli za uhimilishaji na udungaji wa vichocheo vya kufanya ng'ombe waonyeshe dalili za joto(oestrous synchronisation).
Shughuli za upimaji wa ng'ombe waliobainishwa kwa ajili ya uhimilishaji itaanza tarehe 1 Desemba,2017,na ABEA itashirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kuboresha mbari za ng'ombe Wilayani.Kauli mbiu ya ABAE ni "Ongeza tija na uzalishaji wa maziwa kwa kutumia mbari bora na kuwezesha ng'ombe wako kupata ndama kila mwaka kwa kutumia huduma za uhimilishaji".
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved