Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kyerwa Mwl. Ramadhani Marwa amefungua mafunzo hayo ambayo yatafanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa Halmashauri kuanzia leo tarehe 4 hadi 6 Agosti 2025.Akiongea na Washiriki hao, Mwl. Marwa amesema "mnategemewa katika utendaji wenu, muwajibike ipasavyo katika kipindi chote cha utumishi wenu wa kuitumikia Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi hadi hapo tutakapokamilisha jukumu hili la uchaguzi mkuu."Mafunzo haya yanajumuisha washiriki 48 ambao ni Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Kata kutoka katika Kata zote 24 za Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ambao wameapa kiapo cha kuitumikia kazi hiyo kwa kipindi chote
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved