WASAJILI WASAIDIZI wanaoendelea na mafunzo ya usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano wamegawiwa simu janja ambazo zitawasaidia katika kusajili taarifa za watoto kwa njia ya mtandao.
Mafunzo hayo ya siku tatu yanayoendelea katika ukumbi wa CCM wilayani Kyerwa yakitolewa na wataalamu kutoka RITA makao makuu ya Taifa Tanzania Bara, RITA Mkoa wa Kagera na wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya ya Kyerwa leo yamefikia siku ya pili na kwa wasajili wasaidizi kufundishwa namna ya kingiza taarifa katika mfumo baada ya jana na leo mapema kuolekezwa namna ya kuingiza taarifa za watoto katika fomu maalumu za uasajili.
Simu janja ambazo zimeunganishwa na mfumo wa eRITA zimetolewa kwa udhamini wa kamuni ya simu za mkononi ya Tigo ambayo ni moja ya wadhamini wa programu inayoendelea nchi nzima. Na kwa upande wa Wilaya ya Kyerwa imetoa simu 63 kwa wasijili wasaidizi, ambapo watendaji wa kata wamepewa simu 23 na 39 kwa wahudumu wa afya.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved