Wananchi wa Kijiji cha Migina, kata ya Songambele wamedhamilia kujenga Zahanati ya Kijiji chao ili kuepuka adha ya kwenda zahanati ya Songambele kupata huduma za matibabu. Hayo yamebainika baada ya Serikali ya Kijiji kununua eneo la ujenzi wa Zahanati hiyo lenye ukubwa wa takribani ekari moja kutoka kwa mwananchi.Kijiji cha Migina kwa muda mrefu kimekuwa kikitegemea Zahanati ya Songambele na Kituo cha Afya Nkwenda kwa ajili ya kupata huduma za matibabu hali ambayo ni kero kwa wakazi wa eneo hilo kutokana na umbali wa mwendo mrefu na ubovu wa barabara hasa nyakati za masika.
Akizungumza wakati wa kufanya ukaguzi pamoja na kuchukua jira (coordinates) za eneo linalopendekezwa kujengwa Zahanati, Afisa Ardhi wa Wilaya ya Kyerwa Ndugu Richard Mayiku aliwashauri Kamati ya Serikali ya kijiji waendelee kununua ardhi angalau zifike ekari sita ambazo ndiyo takwa la kisheria kwa ajili ya kupata kibali cha kuanzisha Zahanati. Aidha aliwashukuru wananchi wa Migina kwa hatua hiyo.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved