Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa imepokea walimu 10 kati ya 14 waliopangwa kufundisha masomo ya Sayansi kwa kidato cha tano na sita katika Wilaya ya Kyerwa kwa udhamini wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania ERB.
Kwa lengo la kuibua wahandisi wenye tija kuanzia ngazi ya chini Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania imedhamini walimu hao wa Mkataba watakaofundisha masomo ya Hisabati, Fizikia, Kemia, na Baiolojia katika shule zenye taasusi (combination) za sayansi kwa ngazi ya kidato cha tano na sita katika Wilaya ya Kyerwa ambazo
ni Shule ya Sekondari Kyerwa na Lut. Gen. Silas Mayunga iliyopo kata Bugomora.
Akiwapokea walimu hao Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Mwl. Mayala Sengerema ameishukuru Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB) na kuwaomba walimu hao kwenda kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufaulu hasa katika masomo ya sayansi ambayo wanafunzi wengi huyakimbia kwa dhana ya kuwa ni masomo magumu.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved