“WAJA” WAHIMIZWA KUHAMASISHA WANANCHI ULAJI WA MBOGAMBOGA.
Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (WAJA) wameagizwa na ndugu Shadrack Mhagama kuwa himiza wananchi kushiriki katika ulimaji na matumizi ya vyakula vya mboga mboga. Hayo ya mesemwa na ndugu Mhagama ambaye Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kyerwa katika mapitio ya taarifa za kikao cha Kamati ya Lishe kipindi cha Januari hadi Machi 2018 katika ukumbi wa mikutano shule ya sekondari Kyerwa hivi karibuni.
Hayo yameelezwa wakati wa kupokea na kujadili taarifa za idara mtambuka katika kusimamia suala la Lishe Wilayani.
WAJA wameweza kutambua na kusajili jumla ya kaya za walengwa 15,678, ambapo kaya za wajawazito ni 3,215, watoto chini ya miaka 2 ni kaya 10,752 na kaya zenye wajawa zito na watoto chini ya miaka miwili ni 516 tangu mradi wa Mototo Mwelevu ulipozinduliwa hapa Wilayani.
Ili kudhibiti suala la utapiamlo kwa watoto,ni vizuri baada ya miezi 6 ya mwanzo watoto chini ya miaka 2 wapewa vyakula vya kulikizwa vilivyo na mchanganyiko wa mboga mboga ili kupunguza udumavu, alisisitiza ndugu shadrack mhagama.
Aidha Wilaya ya Kyerwa ina jumla ya WAJA 198 katika Vijiji 99 Wilayani kyerwa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved