Wafugaji katika nyanda za malisho ya Ruhita kata ya Kamuli wapelekewa mradi wa ujenzi wa josho la kuogeshea mifugo. Mradi huu unatekelezwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 na unaghalimu jumla ya kiasi cha shilingi 18,000,000 fedha zitokanazo na ufadhili wa Wizara ya Mifugo na uvuvi.
Aidha, kupitia mhandisi wa ujenzi wa Halmashauri, tayari michoro ya usanifu wa mradi huo imeishaandaliwa kwa ajili ya ujenzi. Mradi utakapo kamilika utawanufaisha wafugaji wa eneo hilo ambao mifugo yao ilikuwa ikikabiliwa na changamoto ya magonjwa yatokanayo na kupe.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved