Wadau wa Elimu Wilaya ya Kyerwa wamekutana tar. 23 Agosti 2023 kujadili namna ya kukuza sekta ya elimu kwa kushirikiana na Mfuko wa Kusaidia Maendeleo ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education-GPE) katika ukumbi wa Shule ye Sekondari Kyerwa Modern.
Akiongoza kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe amewahamasisha wadau hao wa elimu kuchanga na kupata kiasi cha kutosha ili kiweze kuendeleza sekta ya elimu katika Wilaya ya Kyerwa na kuunga mkono juhudi za wahisani kutoka nje nchi.
Akitoa wasilisho la mradi huo wa GPE, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kyerwa, Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Wilaya ya Kyerwa Mwl. Ndabazi Stephano amesema nchi ya Tanzania ni mnufaika wa mpango ambao ushatolewa kwa awamu mbili tofauti na awamu ya tatu imepewa aina tatu ambazo aina mbili tayari Tanzania imenufaika nayo.
Ameeleza katika aina ya tatu GPE wameweka masharti ya Dola Moja ya Marekani sawa Dola Moja ya Marekani (USD I = USD I) ikizitaka kila nchi mnufaika kuchangia kiasi sawa na kile kitakachotolewa na hivyo kuwahimiza wadau wa elimu kuchangia kiasi kikubwa ambacho kitapelekea kupata hela nyingi za wafadhili hao na kuboresha elimu.
Kwa upande wao wadau wa elimu wameupokea mpango huo na wameonyesha mwamko kwa kuanza kuchangia na kujaza fomu za mikataba ya ahadi zao ambayo jumla wameahadi kuchangia Tsh 18,286,500/= kwa wadau waliokuwepo ukumbini hapo na wadau wengine wa Wilaya ya Kyerwa wataendelea kuchangia kabla mikataba ya ahadi kutumwa ngazi ya mkoa tar. 25 Agosti 2023.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved