Umoja wa wanakikundi cha wachimba madini Kyerwa umemuomba Mheshimiwa Stanslaus Nyongo-Naibu waziri wa Wizara ya Madini,kutambuliwa kwa shughuli zao ikiwepo kupatiwa leseni za uchimbaji mdogo mdogo.Hayo yamesemwa hivi karibuni ambapo Mheshimiwa Nyongo alipotembelea mgodi wa Nyaruzumbura uliopo Wilayani Kyerwa mkoani Kagera leo tarehe 28 februari,2018.
Mheshimiwa Nyongo amewahimiza wachimbaji hao kufuata sheria na taratibu za uchimbaji ili wajikwamue kiuchumi na Serikali iweze kupata mapato kupitia kodi.Katika kusisitiza hilo Mheshimiwa Nyongo,amemuomba Mheshimiwa Kanali Mstaau Shabani I.Lissu Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa kuimarisha ulinzi dhidi ya utoroshwaji wa madini unaofanywa na wafanyabiashara wachache wasio waadilifu.Katika kuhitimisha Mheshimiwa Naibu Waziri,aliwaahidi wachimbaji hao kuwa leseni zitaanza kutolewa na kuhuhishwa hivi karibuni mara baada ya Tume ya Madini itakapo ana kuanya kazi ake rasmi.
Aidha madini ya bati yanayopatikana Wilaya hii,yamekuwa yakitumika katika kutengenezea bidhaa za vifungashio(alluminium foil) vya vyakula.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved