Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa imepokea vifaa vya umeme wa jua (solar system) vyenye thamani ya Milioni 62 kutoka katika Kampuni ya Mavuno Project yenye makao yake Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera ili kuwezesha vituo hivyo kuwa na umeme wa uhakika na kutoa huduma muda wote.
Akipokea vifaa hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa SACF. James John ameishukuru kampuni ya Mavuno Project kwa kutoa vifaa hivyo na kusema kuwa vitasaidia kwa Madaktari na watoa huduma wa vituo hivyo kutoa huduma muda wote.
“Lengo hasa ni kuweza kukabiliana na changamoto ya umeme hasa muda wa usiku. Kama mnavyofahamu umeme tunao na kuna wakati unakatika, kwa ‘solar panel’ zinatupa ‘assurance’ ya kufanya kazi muda wote na kuendelea kuwahudumia wagonjwa haswa Wamama wajawazito wakati wa kujifungua,” Ameeleza DED.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Dkt. Msafiri Lewanga ameeleza, vituo vya afya ambavyo vitanufaika na huduma hiyo kuwa ni vituo vya Rutunguru, Mabira, Murongo na Kamuli ambavyo vitapelekea Madaktari na wahudumu wa afya kufanya kazi kwa ari, moyo na weledi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Mavuno Project Bw. Charles Bahati amesema wameangalia vituo ambavyo vinatoa huduma kwa watu wengi na hivyo kutoa solar panel 16, betri 8 na charger controller 4 ambazo zitasaidia mwanga, kuchaji simu na matumizi ya Komputa na kuahidi kuendelea kushikirikiana na Wilaya Kyerwa kwa wakati ujao.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved