TUNATEKELEZA: Baada ya Serikali kuridhika na utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa Kituo cha Afya Murongo wilayani Kyerwa kwa kutumia Sh. Milioni 400 za awamu ya kwanza, Serikali ilitoa fedha nyingine Sh. Milioni 400 kwa ajili ya upanuzi wa Kituo kingine cha Afya Kamuli. Fedha hizi zimeelekezwa katika ujenzi wa Wodi ya wazazi, Maabara, Chumba cha Upasuaji na nyumba ya Mganga. Aidha ujenzi huo umeshaanza (kama inavyoonekana katika picha) na unaendelea vizuri zhini ya usimamizi madhubuti kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kwa kushirikiana na Jamii itakayonufaika na Mradi huo. Serikali kupitia Mkurugenzi Mtendaji inaendelea kutoa wito kwa jamii husika kuendelea kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa miradi ya maendeleo pale itakapohitajika.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved