Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe ametembelea Kata ya Businde kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za Wananchi zinazowakabili katika mazingira yao huku akiwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanaandikisha watoto wao wanaotakiwa kujiunga na shule.
Ukesefu wa maji safi na salama, barabara mbovu na makaravati yasiyopitika muda wote, kutofikiwa na umeme kwa baadhi ya vijiji, kutokuwa na Vitambulisho vya taifa, migogoro ya ardhi, umaliziaji wa miundombinu ya elimu na afya ni miongoni mwa kero zilizojitokeza na kutolewa ufafanuzi na wataalam walioambatana na Mkuu wa Wilaya huku kero zingine zikichukuliwa kwa ajili ya utekelezaji zaidi.
Aidha katika hotuba yake Mhe. Msofe amewasisitiza wazazi na walezi wa Kata ya Businde na Wilaya ya Kyerwa kwa ujumla kuhakikisha wanaandikisha watoto kabla ya muda wa uandikishaji kuisha, kwani elimu ni haki ya msingi kwa mtoto.
“Mtoto anahaki ya kupata elimu, lakini mzazi anawajibu wa kuhakikisha mtoto wake anapata elimu. Nimeshatoa maelekezo polisi, tumeongea na vyombo vingine kwamba kipaumbele chetu sisi ni watoto waende shule kwa hiyo mzazi ukikamatwa hakuna wa kukutetea, ukienda polisi wamejipanga na ukienda mahakamani wamejipanga sijui utenda wapi tena.”
“Mkaambizane wale wanye watoto wao ambao bado wapo nyumbani wawapeleke shule, kama mtoto wako anaumri wa kwenda shule alafu umemuweka nyumbani hilo pia ni kosa. Kwa hiyo watakapoanza kuwasaka na kukuta mtoto mwenye umri wa kwenda shule huyu pia bebeni.” Ameeleza Mhe. Msofe.
Wilaya ya Kyerwa imetoa mwisho wa kuwaandisha watoto wa darasa la awali, darasa la kwanza na kuripoti kidato cha kwanza kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na sekondari ni tarehe 30 Januari 2024 na ifikapo tarehe 3 Februari 2024 utaanzishwa msako wa nyumba kwa nyumba ili kubaini watoto ambao hawaandikishwa na wazazi au walezi wao kuchukuliwa hatu za kisheria.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved