Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na kamati ya miradi wilaya ya Kyerwa ikiongozwa na mkuu wa Wilaya, Mhe. Zaituni Msofe, imekagua miradi na maeneo mbalimbali wilayani humo, kama sehemu ya maandalizi ya ujio wa mwenge wa uhuru mwezi Agasti mwaka huu.
Kamati hizo zimetembelea jumla ya miradi nane ambayo itatembelewa na mwenge kwa ajili ya kuwekewa jiwe na msingu na baadhi itazinduliwa. Pia maeneo mawili ya Kijiji cha Mabira, sehemu ambayo utapokelewa mwenge wa uhuru na eneo ambalo utalala mwenge wa uhuru katika viwanja vya standi ya mabasi ya Nkwenda.
Miradi miwili ambayo iko makao makuu ya Wiliya Kyerwa, Rwenkorongo ambayo ni barabra ya lami yenye urefu kilometa 1.2 uliogharimu milioni 500 fedha za mfuko wa jimbo na kiwanda cha kukoboa kahawa ambacho kinamilikiwa na chama cha ushirika cha msingi cha mkombozi limited ambacho kinauwezo wa kukoboa tani sita kwa saa.
Kamati hizo zimetembelea miradi mitatu katika kata ya Nkwenda kwa kuanza na eneo la upandaji miti 500 (ya matunda 200 na ya mbao 300) itakayo pandwa katika shule ya Kaaro, ukaguzi wa madarasa matano katika shule ya sekondari Nkwenda na jingo la wodi ya wanaume mchanganyiko katika kituo cha Afya Nkwenda.
Aidha kamati ilitembelea miradi ya kitalu cha kuotesha miche ya miti mchanganyiko ya matunda na mbao, unaosimamiwa Taasisi ya Misitu Tanzanzia (TFS), kukundi bodaboda Juhudi chenye pikipiki kumi ambazo zilinunuliwa kwa fedha za mkopo zilizotolewa na Halmashauri, mradi wa Maji katika kijiji cha Kagenyi-Omukalinzi pia mradi wa mabanda maonyesho, katika kijiji cha Nyakatuntu.
Mhe. Msofe pamoja na kamati ilikuwa ikitoa maagizo na maendekezo kwa wahusika wa kila mradi na kutaka yashugulikiwe mapema iwezekanavyo ambayo yalitolewa kuingana na hali ya mradi husika.
Alisisitiza swala la usafi wa mazingira katika maeneo yote ya miradi, kuhakikisha nyaraka zote za kumbumbu ziwekwe vizuri na kwa upande wa vijana wa Bodaboda wahakikishe wanafuata taratibu za usalama barabarani na kuhakikisha wote wanapitia mafunzo ya udereva na kupatiwa leseni.
Mkuu wa wilaya aliambatana na mwenyekiti wa wilaya, Mkurugenzi mtendaji, Katibu tawala wa wilaya na wakuu wa idara na vitengo.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved