Wawakilishi wa Shirika la Maendeleo Duniani-UNDP hivi karibuni watembelea na kukagua miradi inayofadhiliwa na Shirika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa. Msafara huo uliongozwa na Ndg, Abbas Kitogo kutoka Shirika la UNDP na kutembelea miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi nne zinazoendelea na ujenzi wa vyumba hivyo. Shirika kwa kushirikiana na serikali ya Afrika Kusini imefadhili ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa katika shule za msingi za Masheshe, Nyamiyaga, Kikukuru na Nyakatuntu. Wakati wa ukaguzi waliweza kushauri mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kuzingatia ujenzi ambao ni kinzani na majanga kama Tetemeko la Ardhi. Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kupitia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri imeshukuru kwa ufadhili huo na kuahidi kutekeleza mradi kwa weledi mkubwa na kwa viwango vinavyotakiwa na pia kuwakaribisha tena kila watakapoweza kufadhili kwa kuwa mahitaji bado ni makubwa hasa sekta za Elimu na Afya.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved