Kituo cha Afya Murongo kilichopo kata ya Murongo, Wilayani Kyerwa kinafanyiwa ukarabati mkubwa ambapo hadi sasa ujenzi umefikia 90% kukamilika.Hayo yamebainishwa na Mhandisi wa ujenzi Halmashauri ya Kyerwa ndugu Juma Magotto alipokuwa akihojiwa na mwandishi wetu.
“Napenda kuishukuru Serikali ya awamu ya tano, kwa kutuwezesha fedha kiasi cha shilingi milioni mia nne kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa kituo hiki cha Afya”, alisisitiza ndugu Magotto.
Ujenzi wa kituo hiki ulianza mnamo tarehe 28 Februari,2018 ambapo maeneo yaliyotengenezwa ni pamoja na ukarabati na upanuzi wa jengo la upasuaji(Thearter),ujenzi wa wodi ya wazazi(Maternity ward),ujenzi wa maabara,ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti(Mortuary) , na ujenzi wa nyumba ya mganga.
Kituo cha afya Murongo kwa mwaka kinahudumia takribani wagonjwa 18,733,hivyo uboreshaji wa miundombinu hii utachochea ufanisi wa utoaji na upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa maeneo jirani.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved