Katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Tar. 23 Aprili 2024 katika Wilaya ya Kyerwa umefanyika usafi wa mazingira na kupanda miti katika Kituo cha Afya Nkwenda.
Akiongoza Watumishi wa Umma pamoja na Wananchi Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe amewataka kuendelea kutunza mazingira kwa faida ya kizazi kijacho kwani Wilaya ya Kyerwa imebarikiwa kuwa na hali nzuri ya hewa na inatakiwa kutunzwa.
Mhe. Mkuu wa Wilaya amesema wananchi wote ambao wamegawiwa miti wanatakiwa kuitunza na kuwahimiza wafike katika Ofisi za TFS zilizopo Rubwera ili wakapewe miti ya kupanda katika maeneo yao na waendelee kutunza mazingira.
“Utunzaji wa mazingira ni suala nyeti sana, tusione tunasherehekea hapa tunapata mvua mara mbali kwa mwaka hii yote ni kwa sababu kuna waliokuwa wamepanda miti na wakaitunza kwa hiyo na sisi tumepewa miti, na mingine tukachukue tukapande na tukaitunze ili kuhakikisha kizazi chetu kinachokuja baadae wanaendelea kupata hali ya hewa kama tunavyopata sisi, ameeleza Mhe. Msofe.
Mkuu wa Wilaya pia amewatembelea akinamama waliojifungua na wanaotarajia kujifugua katika kituo cha Afya Kwenda kwa lengo la kuwajulia hali na kuongea nao ikiwa ni moja ya shughuli zilizopangwa kufanyika katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akiwafariji kwa zawadi.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru inasema, “miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tumeshikamana na Tumeimarika kwa Maendeleo ya Taifa Letu.”
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved