Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe amewataka wajumbe wa kikao cha kamati ya lishe kupambana na hali ya watoto wanaozaliwa chini ya uzito wa 2.5Kg. baada ya kupokea na kujadili taarifa utekelezaji wa mkataba wa Lishe kwa Wilaya ya Kyerwa katika kipindi cha robo ya pili ya kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba 2024/2025.
Hayo yamebainishwa leo tarehe 06 Machi 2025 katika kikao cha kujadili taarifa hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ambapo Mkuu wa Wilaya amewataka wajumbe wa kikao hicho kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili kuhakikisha watoto wanazaliwa wakiwa na afya njema na uzito wa zaidi ya 2.5Kg.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa, sababu zinazochangia kuwepo kwa watoto wanaozaliwa na uzito mdogo ni akinamama wengi kutokutumia dawa za kuongeza damu na kuboresha afya ya mtoto akiwa tumboni kwa madai ya kuwa zinawafanya wanajihisi vibaya, huku wengine kutokufuata maelekezo ya wataalam wanapopewa kipindi cha kuhudhuria kliniki.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved