Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Kyerwa umepitia na kujadili hoja za taarifa ya ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) za mwaka wa fedha 2021/2022 ambacho kimefanyika tar. 16 Juni mwaka huu.
Katika kikao hicho Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Bw. Toba Nguvila akimwakilisha mkuu wa Mkoa Kagera ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kwa kupata hati safi na kutoa rai ya kuendea kuwa na sifa hiyo.
Bw. Nguvila amesema halmashauri ilipata hoja 16 katika mwaka wa fedha 2021/2022 ambazo ziliibuliwa na Mkaguzi mkuu wa serikali, ambazo sita zimefungwa na hoja kumi bado ziko katika utekelezaji na kuwataka wahusika kushughulikia hoja zilizobaki ili zifungwe.
Aidha Bw. Nguvila amewataka Madiwani na watumishi wa halmashauri kudhibiti magendo ya utoroshaji wa kahawa kwani unaikosesha halmashauri mapato.
“Sisi tuwe chanzo cha kudhibiti magendo na tusiwe chanzo cha magendo … Madiwani, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji, msiwe wapole kwenye wizi na ubadhilifu wa fedha za umma”, Alisema Bw. Nguvila.
Vile vile amewaagiza madiwani wote kushirika kikamilifu katika mbio za mwenge wa uhuru 2023 ili kuisadia wilaya ya Kyerwa kupata alama nyingi na awali alianza na zoezi la kutembele miradi yote itakayotembelewa na mwenge wa uhuru na kujionea hali nzuri ya miradi hiyo.
Aidha awali akizungumza na baraza Mkuu wa Wilaya Bi. Zaituni Msofe amewahimiza waheshimiwa madiwani na watumishi wote wanaohusika na kukusanya mapato waongeze bidii kwa kuwa huu ni msimu wa kuvuna kahawa na dio zao kuu linaloongoza kwa mapato katika wilaya ya Kyerwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Bahati Lekayo ametoa rai ya kutosafirisha kahawa usiku ili kupunguza mianya ya magendo ya utoroshaji wa kahawa jambo ambalo limeungwa mkono na wajumbe wote wa baraza.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved