Katibu Tawala wa Wilaya ya Kyerwa Bw. Mussa Gumbo, Julai 16, 2025 amefanya ziara katika Kijiji cha Rwenkende Kata ya Kibingo ikiwa ni mwendelezo wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Wilaya ya Kyerwa.
Akizungumza na Wananchi waliojitokeza katika Mkutano huo amewataka kuacha kuchoma moto ovyo katika mazingira yao hasa katika kipindi hiki cha kiangazi ambapo wananchi wanatarajia kuanza shughuli za kuandaa mashamba.
“Kuna tabia ya kuchoma moto hovyo, hiyo tabia ikome mara moja kwa sababu mtachukuliwa hatua za kisheria. Tusitegemee Mkuu wa Wilaya au Mtendaji wa Kata au Afisa Tarafa aje, wanaochoma moto tunawajua, kwa hiyo ukiona mtu anachoma moto toa taarifa, sisi tutakuja kumkamata na kuchukua hatua za kisheria,” ameeleza Bw. Gumbo.
Aidha Bw. Gumbo amewataka wananchi kuendelea kuchangia miradi ya maendeleo, kuisimamia na kuitunza ili iendelee kutoa huduma na kuwanufaisha wananchi wanaoitumia miradi hiyo.
Vile vile amewataka wananchi kuendelea kuchangia chakula shuleni, kulinda na kuwafundisha watoto maadili mema ili kuendelea kuwa na kizazi bora cha sasa na cha baadae huku akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi pamoja na kutunza amani ya nchi.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved