Mkuu wa Wilaya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe leo Tar. 11 Aprili 2024 amewatembelea na kuwapa mkono wa Eid Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum wanaosoma katika shule ya Sekondari Mabira.
Akitoa mkono wa Eid Al Fitr kwa niaba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Msofe amesema lengo la zawadi hizo ni kufurahia na kujumuika kwa pamoja na Wanafunzi hao katika kipindi hiki cha Sikukuu.
“Hakika mama ni mama, aliona kwa vyovyote iwavyo asikae mwenyewe makao makuu ya nchi akawa na furaha ya kula Eid lakini watoto wake huku Wilayani hawana hiyo furaha, hivyo alituagiza tuwatafute nyinyi walau tuweze ‘kushare’ furaha hii ya Eid katika siku hii adhimu.
“ametuelekeza tuje kwenu tuwaletee mahitaji ambayo na nyinyi kwa namna moja au nyigine mnaweza kufurahia na kusherehekea sikukuu hii ya Eid.” Ameeleza Mhe. Msofe.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Mabira Mwl. Danford Nuvye amesema Shule hiyo ina wanafunzi wa Kiume 86 wenye mahitaji maalum na kushukuru ugeni wa Mkuu wa Wilaya kufika katika shule yao na kuwajali wanafunzi hao kwani jambo hilo linawatia moyo na litepelekea hata kuongeza ufaulu wa Wanafunzi hao.
Pia wanafunzi hao wamemshukuru Mhe. Rais pamoja na Muwakilishi wake Mhe. Mkuu wa Wilaya na kusema kuwa tendo hilo limewafurahisha na kuahidi kufanya vizuri katika masomo na kutimiza malengo yao.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved