Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Bw. Mathew Rufunjo ametoa elimu juu ya kutumia mfumo mpya wa TAUSI ambao humsaida mfanyabiashara kupata leseni kwa njia ya kidigitali.
Hayo yamefanyika katika kata ya Nkwenda wilayani Kyerwa ambapo amekutana na baadhi ya wafanyabiashara na kuwaeleza namna ya kutumia mfumo huo pamoja na faida zake kwa wafanyabiashara wa kisasa wanaoendana na ulimwengu wa kidigitali.
“Mfumo ambao unaweza kumsaidia mfanyabiasha kupata leseni za biashara, leseni za vileo, ushuru wa huduma, leseni za hoteli, kodi ya pango na vibali vya ujenzi kwa njia ya kidigitali na bila kufika katika ofisi za halmashauri.
Ukiwa na simujaja yako, namba ya NIDA, TIN namba na bando lako unaweza kujisajili kupitia link https://tausi.tamisemi.go.tz wewe mwenyewe bila kufika katika ofisi za halmashauri.” Alsema Bw. Rufunjo.
Aidha amewataka baadhi ya maafisa usafirishaji wa pikipiki maarufu kama bodaboda na bajaji ambao hawana leseni, kuhakikisha wanakata leseni za usafirishaji kwani kufanya shughuli hiyo bila leseni ni kunyume na sharia na wanaweza kuchukukuliwa hatua.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved