Leo Desemba 01, 2024,Tanzania imeungana na Mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha Siku ya UKIMWI Duniani.
Katika Mkoa wa Kagera Maadhimisho hayo yamefanyika katika Viwanja vya Standi ya Nkwenda Wilaya ya Kyerwa.
Akiongoza maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwasa ametoa rai kwa wananchi na kuwakumbusha kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa UKIMWI.
"Tanzania bila UKIMWI inewezekana lakini pia Kagera bila UKIMWI inawezekena" amesisitiza Mhe. Msofe wakati akizungumza na wananchi waliofika katika viwanja hivyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudhibiti UKIMWI Wilaya ya Kyerwa Mhe. Clarence Rugimbana amesema Wilaya ya Kyerwa imepunguza maambuzi ya VVU kutoka asilimia 0.8 kwa mwaka 2023 hadi asilimia 0.7 kwa mwaka 2024.
Aidha amesema ataendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali pamoja na wadau wengine ili kuendelea kupambana na VVU pamoja na ugonjwa wa UKIMWI katika Wilaya ya Kyerwa.
Kauli mbiu ya Maadhimisho haya kwa mwaka 2024 ni "Chagua Njia Sahihi, Tokomeza UKIMWI"
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved