Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe ametoa rai hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kihanga Kata ya Isingiro tarehe 15 Julai 2024 wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Mhe. Mkuu wa Wilaya amesema kutokana na tukio la kuuliwa kwa Albino lilitotokea hivi karibuni katika Wilaya jirani ya Muleba amewataka wananchi, wazazi, ndugu jamaa pamoja na viongozi kushirikiana katika kuwalinda watu hao dhidi ya watu wenye nia mbaya ambao wanataka kuwadhuru watu wenye ulemavu wa ngozi.
“Nafahamu hivi karibuni katika Wilaya Jirani ya Muleba kulitokea huo mkasa, Ndugu zangu niwaambie tu wale ni binadamu kama walivyo binadamu wengine, wala hakuna uhusiano wa Albino na wewe kutajirika, tuache kukatisha uhai wa hawa watoto, tuache kukatisha uhai wa ndugu zetu, tuache Imani potofu.” ameeleza Mhe. Msofe.
Aidha kero mbalimbali zilizoibuliwa katika mkutano huo ni pamoja na ukosefu wa maji safi na salama, kutokuwekwa matuta katika kivuko cha barabara katika eneo la shule ya Msingi Kihanga, kutofikiwa na umeme katika baadhi ya Vitongoji, kutokuwa na Vitambulisho vya taifa, upungufu wa Walimu, umaliziaji wa miundombinu ya afya pamoja na michango ya lishe.
Vile vile baadhi ya wanufaika wa TASAF kutolewa huku hali zao zikiwa duni, wezee kutonufaika na shirika la kusaidia wazee huku likiwatoza ada ya usajili na biashara ya butula ni miongoni mwa kero zilizojitokeza na kutolewa ufafanuzi na wataalam walioambatana na Mkuu wa Wilaya huku kero zingine zikichukuliwa kwa ajili ya utekelezaji zaidi.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved