Timu ya wataalam toka Halmashauri ikiongozwa na Afisa Ardhi wa Wilaya ndugu Richard Mayiku mnamo tarehe 7 septemba,2017
walitembelea eneo la mpango mji wa Wilaya eneo la Rubwera ili kufanya tathmini na mapitio ya eneo lililotengwa kwa ajili ya maziko.Suala hili limekuja kutokana na kuwapo na muitikio mdogo wa wananchi kuzika katika eneo ambalo limepangwa kwa madai mbalimbali ikiwamo kuwa eneo tengwa halifai kwa maana kwa kiasi cha ekari 5 kati ya ekari 11 zilizotengwa kwa ajili ya makaburi zinatwama maji kipindi cha masika.
Aidha,naye ndugu Yasin Mwinory-Afisa mazingira Wilaya ya Kyerwa,alibainisha kuwa kwa mujibu wa sheria ya Afya ya Jamii ya mwaka 2009,kifungu cha 126,kifungu kidogo cha 5 inasisitiza kuwa eneo la maziko linatakiwa kuwa mita 100 mbali na maeneo ya makazi ya watu,na vyanzo vya maji.Hivyo alishauri yatafutwe maeneo mengine mbadala yanayokidhi viwango kwa mujibu wa sheria,kanuni,na taratibu za afya na mazingira.
Kwa miaka mingi utamaduni wa wananchi wa Wilaya ya Kyerwa wamekuwa wakizika ndugu,jamaa,na wapendwa wao katika maeneo ya mazaki ya nyumbani kwa marehemu wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo ni kutomtelekea marehemu/kumtupa tofauti na kwenda kumzika katika makaburi ya jumuiya.
Timu hii inaendelea kubaini maeneo mengine ya maziko katika miji ya Nkwenda,Mabira,Isingiro,na Murongo kubaini changamoto zinazojitokeza katika maeneo hayo na kutoa suruhisho la namna bora ya kutenga maeneo hayo.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved