Mdau wa Maendeleo Wilaya ya Kyerwa, Meneja wa kampuni ya Karagwe Estate Bi. Devotha Daniel amegawa taulo za kike pisi 300 kwa wanafunzi wa shule za Sekondari za Kyerwa Modern na Kyerwa pamoja na Shule ya Msingi Kyerwa ikiwa ni moja ya shughuli anazozifanya katika kipindi hiki cha kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
“Katika kuelekea siku ya wanawake Duniani nimetoa taulo za kike pisi 300 najua ni kidogo ila zitawasaidia, nimetoa pia mipira 2 ya ‘netball’, na wavulana nimewaletea mipira 2 ya ‘football’ ikiwa na lengo la kuhamasisha michezo kwani michezo ni afya” amesema Bi. Devotha.
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ambaye pia alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Bw. Goldian Regeimukamu amemshukuru Mdau huyo na kusema taulo hizo zitawasaidia watoto kusoma kwa uhuru na utulivu, huku akiwakaribisha wadau wengine kuunga mkono juhudi hizo na kutoa misaada kama hiyo ili kupunguza utoro, kuongeza ufaulu na kujiamini kwa watoto wa kike shuleni ikiwa ni njia ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuinua elimu nchini.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved