Shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake makuu nchini Ujerumani la Jambo Bukoba limeendesha mafunzo ya michezo kwa walimu wa shule za msingi hapa Wilayani kuanzia tarehe 23-27 oktoba,2017.Mafunzo haya yaliyofanyika katika kituo cha shule ya msingi Nyakatera,iliyopo katika tarafa ya Murongo,kata ya Bugomora,yameratibiwa na meneja mradi wa Jambo Bukoba kwa kushirikiana na mratibu kata Bugomora.
Katika kilele cha mafunzo hayo,mgeni rasmi ndugu Pascal Mayala,afisa utamaduni wa Wilaya aliwaga zawadiya mpira mmoja wa miguu kwa kila shule,cheti cha ushiriki na skafu kwa kila mshiriki wa mafunzo.
Aidha,mafunzo hayo pia yamelenga kuboresha miundo mbinu mashuleni,uelimishaji juu ya masuala ya UKIMWI mashuleni,kutoa stadi zamaisha kwa wanafunzi,na kuhimiza usawa wa kijinsia mashuleni.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved