MKUU wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amefanya ziara Wilayani Kyerwa ikiwa ni mwendelezo wa kutembelea Wilaya zilizoko katika Mkoa wa Kagera ili kukagua na kupata taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya hizo.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa alitembelea miradi ya ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri na hospitali ya Wilaya Kyerwa ambayo ameridhishwa na kupongeza usimamizi mzuri wa miradi hiyo na kuwasisitiza wahusika wa miradi kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na kusimamia miradi inayotekelezwa kwa fedha nyingi zinazotolewa na serikali ya awamu ya sita.
Aidha Mkuu wa Mkoa alifanya kikao cha ndani na wakuu wa idara na vitengo vya halmashauri na taasisi mbalimbali za serikali zilizopo wilayani Kyerwa na kupokea taarifa mbalimbali za usimamizi na utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinazofanywa na wataalamu hao na baada ya hapo, alizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Nkwenda ambapo alipoka kero mbalimbali za wananchi na kuzitolea ufafanuzi.
Kero hizo zililenga katika uhaba wa maji safi na salama, changamoto ya barabara ya lami, umeme kutokufika katika baadhi ya vijiji na kukatika mara kwa mara, upungufu wa watumishi ikiwemo askari polisi, ukosefu wa namba na vitambulisho vya NIDA. Kero ambazo alizipokea na kutolewa ufafanuzi na kuahidi kuzifanyia kazi.
Vile vile amepokea maombi ya Nkwenda kuwa mji mdogo pamoja na kupatiwa chama cha ushirika cha Wilaya kwa ajili ya kukusanya kahawa na kuahidi kuyafanyia kazi maombi hayo kwa kushirikiana na wataalamu pamoja Mhe. Mbunge wa Jimbo la Kyerwa na pia kwa kuyafikisha sehemu husika ili kuongeza msukumo wa mambo hayo kushughulikiwa kwa haraka.
Pia katika hotuba yake Hajjat Fatma amewataka wananchi waache kutumia vibatali ambavyo hupelekea madhara makumbwa na mauaji ya kuungua moto kwani utumaduni wa watu wa Kagera hupenda kutandika nyasi ambazo ni rahisi kushika moto na kuwataka kutumia nishati mbadala. Pia na kuzingitia ulaji wa lishe bora, Pamoja na kudumisha umoja upendo na pia kuwataka wanakyerwa kujiandaa na mapokezi ya ujio wa mwenge wa uhuru 2023 na kushiriki kikamilifu.
Kuhusu Magendo ya kahawa amesema, “Serikali iko makini, wanaotorosha kahawa wanahujumu uchumi wa nchi, kwanza wanatukosesha fedha za kigeni, wanatukosesha ushuru wa mapato ya ndani zile asilimia ambozo tungepata hatupati, lakini pia wanarudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu kwa hiyo tutakao wakamata watatumika kuwa mfono kwa wengine ambao wana nia ovu.”
Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Toba Nguvila na baadhi ya watalamu na kamati ya ulinzi na usalama mkoa ambao walipokelewa na wenyeji wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved