Ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa. Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa inatekeleza Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya katika eneo la mji la Rubwera. Ujenzi huu unatekelezwa na SUMA JKT baada ya Halmashauri kuvunja Mkataba wa awali na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) baada ya kusuasua katika ujenzi wa Ofisi hiyo. Halmashauri mpaka sasa imekwisha pokea fedha Shilingi Bilioni moja na Milioni Arobaini na tano (1,045,000,000) kwa ajii ya Mradi huo. Aidha imekwisha tumia Milioni mia moja na sita (106,000,000) katika shughuli hiyo. Mradi huo unaendelea chini ya SUMA JKT na maendeleo ni mazuri kama picha iliyopigwa na mwandishi wetu inavyoonekana.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved