Wavuvi wanaovua samaki kwa kutumia nyavu haramu katika Ziwa Karenge wamekusanya pisi 124 za nyavu zenye thamani ya 14,880,000 kwa hiari, na zimeteketezwa na timu ya viongozi wa kiserikali kwa kushirikiana na wavuvi hao leo Tar. 16 Disemba 2023 katika mwalo wa Karenge.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Bw. Prosper Rutakinikwa amewapongeza wote waliotoa nyavu zao kwa hiari huku akiwasihi wavuvi hao kuachana na uvuvi haramu amabao unapelekea kupunguza samaki katika ziwa hilo na akiwataka watoe taarifa za wale wanawauzia nyavu hizo ili waweze kufuatiliwa na sharia kufuata mkondo wake.
Kwa upande wake Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Kyerwa Bw. Johannes Kabakama amesema uvuvi haramu unamadhara makubwa kwa jamii, pamoja na wavuvi wenyewe yakiwemo ya kuua mazalia ya samaki, kuua samaki wachanga, na pia samaki aliyevuliwa kwa nyavu hizo anakua hana ladha na huharibika haraka.
Aidha amesema zoezi hili litakuwa endelevu katika maziwa yote saba yalipo katika Wilaya ya Kyerwa na wakimaliza oparesheni hiyo wataunda vikundi vya ulinzi shirikishi ambavyo vitasaidia kulinda maziwa yote na kupelekea uvuvi wenye tija katika Wilaya ya Kyerwa.
Mwenyekiti wa Wavuvi wa Mwalo wa Karenge Bw. Enshekanabo Banobi amesema watashirikiana na serikali ili kukomesha uvuvi haramu na endapo watambaini mmoja wao anajishughulisha na uvuvi haramu hawatasita kumchulia hatua za kisheria.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved