MKUU wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe amewataka wasimamizi ya miradi mbalimbali itakayotembelewa na Mwenge wa uhuru mwaka 2023, kuandaa nyaraka zote zinazohusika na kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na kamati ya mwenge mkoa waliokuja kukagua miradi hiyo tar. 16 Juni Mwaka huu.
Amesema hayo leo katika kikao cha tatu cha maandalizi ya kuupokea mwenge wa uhuru mwaka 2023 kilichofanyika katika ukumbi wa CCM Wilayani Kyerwa chenye lengo la kujua maendeleo ya utekelezaji wa miradi na ukusanyaji wa michango ambayo inatolewa kwa ajili ya kuwezesha upokeaji wa Mwenge katika Wilaya ya Kyerwa.
Mhe. Msofe amesema wasimamizi wa miradi ambayo itatembelewa na mwenge wa uhuru mwaka 2023 ilitembelewa na kamati ya mwenge mkoa na wasimamizi hao walipewa maelekezo na kuyafanyia kazi kabla ya ujio wa mwenge katika Wilaya ya Kyerwa.
Baadhi ya miradi walitakiwa kuandaa nyaraka zote zinazohusika, zikiwemo za manunuzi, mihutasari ya vikao vya bodi, vyeti vya watoa huduma na usalama vya NEMC, OSHA, na Zima Moto.
Katika uwasilishwaji wa taarifa hizo baadhi ya wasimamizi wa miradi wamefanyiakazi maagizo hayo huku wengine wakiendelea na utekelezaji na wametakiwa kushughulikia kasoro zilizobaki mapema ili kujiweka katika mazingira mazuri kabla ya ujio wa mwenge wa uhuru.
Miradi itakayotembelewa na mwenge wa uhuru kwa ajili ya kuwekewa jiwe la msingi na baadhi kuzinduliwa katika wilaya ya Kyerwa ni Madarasa matano ya shule ya sekondari Nkwenda, eneo la upandaji miti katika shule ya msingi Kaaro, ujenzi wa wodi ya magonjwa mchanganyiko katika kituo cha afya Nkwenda, kutembelea kikundi cha Bodaboda cha BODABODA JUHUDI, Kitalu cha miti Rubwera, barabara ya lami yenye urefu wa km 1.2 makao makuu ya Halmashauri na kiwanda cha kukoboa kahawa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved