Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Kundo Andrew Mathew (MB) akiwasistizia jambo Wataalamu wa Wizara yake mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Rashid Mwaimu (kulia kwake) alipotembelea Maabara ya kompyuta katika Shule ya Sekondari Mabira wilayani Kyerwa hivi karibuni. Katika Ziara yake hiyo aliambatana na Wataalamu wa Taasisi zote zilizopo chini ya Wizara yake ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano TCRA, Shirika la Posta na Shirika la Mawasiliano kwa Umma pamoja na wadau wa Wizara hiyo yakiwemo makampuni ya simu. Mhe. Naibu Waziri alifika shuleni hapo kuona namna TCRA na Shirika la Mawasiliano kwa Umma walivyosaidia upatikanaji wa kumpyuta za kufundishia na kujifunzia katika shule hiyo.
Aidha katika ufafanuzi wa utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na Wizara yake alieleza namna Wizara ilivyoipendelea Wilaya ya Kyerwa kwa kuipa miradi yenye jumla ya thamani ya Sh Bilioni moja na milioni mia Sita ishirini na tano (1,625M) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano katika Kata za Bugomora, Businde, Isingiro, Kibare, Kibingo, Kitwechenkura, Murongo, Rutunguru, Rwabwere na Songambele.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved