Leo 17 Machi 2024 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Ndugu Fadhili Magaya amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Kyerwa yenye lengo la kukagua miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita na Kufanya mkutano wa hadhara kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzishughulikia.
Katika ziara yake Ndg. Magaya amekagua mradi wa ujenzi wa Chuo cha VETA-Kyerwa, Mradi wa Chakalisa-Kimuli, Zahanati ya Rwenyango-Kimuli na Kituo cha Afya Kamuli na Kufanya mkutano wa hadhara katika Kata Kamuli.
Akizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kukagua miradi hiyo Ndg. Magaya ameridhishwa na utekelezaji wa Miradi hiyo ambayo inasimamiwa na Serikali ya Wilaya Kyerwa kupitia Halmashauri, RUWASA na Ofisi ya Mdhibiti Ubora.
Aidha baadhi ya changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa miradi hiyo ametoa maelekezo ili ziweze kushughulikiwa na nyingine amezichukua kwa ajili ya kuzishughulikia na kuleta ufanisi na tija ya miradi hiyo katika kuhudumia wananchi.
Ametembelea pia Mradi wa Shule ya Sekondari ya Zamani Rumanyika iliyopo Kata ya Nkwenda na kujionea hali ya mradi huo ambao umesimama kutoa huduma huku akiwataka Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kyerwa ambao ndio wasimamizi wa mradi huo kusitisha zoezi la kumtafuta mwekezaji nakuahidi kulishughulikia suala hilo ili mradi huo uanze kutoa huduma.
Katika mkutano wa hadhara alisikiliza kero ya wananchi na kuzitolea ufafanuzi huku akitaka suala la uchaguzi wa Viongozi wa Vyama vya Msingi ufuatiliwe ili kuondoa mkanganyiko uliopo katika kuwapata viongozi wa vyama hivyo. Vile vile ameahidi kabla hajamaliza ziara yake ya Mkoa wa Kagera atakuwa amelipatia ufumbuzi suala la Wilaya ya Kyerwa kuwa na Chama chake cha Ushirika.
Ziara hiyo ya siku moja ilikuwa ikijumuisha viongozi wa CCM na Serikali katika Wilaya ya Kyerwa, baadhi ya viongozi wa CCM na Mamlaka za Mkoa pamoja na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Wazazi Taifa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved