Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Mhe. Bahati Henerico ametembelea mradi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Bugara Millennium uliyoko Kijiji cha Rwakabunda kata ya Bugara kwa ajili ya kujionea ukamilishaji wa mradi wa shule hiyo inayotarajiwa kuanza kupokea wanafunzi Januari Mwaka huu.
Mhe. Mwenyekiti ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo na kutoa rai kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri na Mhandisi wa Wilaya kuhakikisha ukamilishaji wa mradi huo na kushughulikia kasoro ndogo ndogo zilizobainika zikamilishwe haraka iwezekanavyo na kushughulikia swala la madawati ya kuanzia kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule hiyo.
Mradi huo wenye thamani ya Tsh 584,280,028 fedha kutoka serikali kuu kwa ushirikiano wa Benki ya Dunia kupitia mradi wa uboreshaji wa elimu ya sekondari nchini (SEQUIP), ambapo majengo 24 yamejengwa ikiwemo ujenzi wa jengo la utawala, vyumba nane vya madarasa, matundu nane ya vyoo, kisima cha maji, kichomea taka, jengo la maktaba na maabara tatu.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved